Watu wengi hawana muda wa kuandaa kifungua kimya asubuhi kwa ajili ya kwao wenyewe au hata familia zao kwa sababu ya kuwa na muda mchache, mawazo ya kuwahi foleni na bosi mkali na vitu kama hivyo. Kuna njia rahisi za kufuata kuhakikisha kila siku unapata kifungua kimya hata kama ratiba yako inabana.
Many people do not have enough time to prepare breakfast in the morning because of tight schedules they have. Here are great ways to prepare eggs in five minutes or less.
- Chemsha mayai mapema/Boil eggs in advance: Unaweza kuandaa mayai ya wiki nzima kwa kuyachemsha hadi yaive kwa dakika kumi na kuyahifadhi vizuri kwenye friji. Mayai yaliyochemshwa yanaweza kuhifadhiwa kwenye friji kwa siku saba bila kuharibika. hivyo asubuhi unaweza kulipasha yai kwa kuliweka kwenye maji ya moto kwa dakika mbili na kulila. Boil enough eggs say on a weekend and store them in a refrigerator. they can be stored for seven days. In the morning, quickly warm the boiled eggs and eat.
- Mayai ya kukaanga/Fried eggs: Kukaanga mayai na rahisi na haraka, weka kikaango na mafuta kidogo ya kupikia, vunja yai na kulikoroga kwenye bakuli, tia chumvi halafu liweke kwenye kikaango kwa dakika mbili huku ukigeuza litakuwa tayari kuliwa. Put a frying pan on a cooker and heat a little oil, beat an egg on a bowl, stir with a pinch of salt and pour it on the pan to fry. In two minutes it will be ready.
- Mayai ya sekunde 60/60 seconds eggs: Kwa wenye 'microwave', vunja yai liweke kwenye kikombe au bakuli linaloweza kuwekwa kwenye microwave, ifunge na weka joto la juu kabisa halafu acha kwa sekunde 60. Toa kikombe chenye yai lililoiva, weka chumvi, changanya na litakua tayari kuliwa. Just crack an egg into a microwave safe cup and zap on high for one minute. Stir, season and breakfast is ready.
No comments:
Post a Comment