Wednesday, March 16, 2016

Jinsi ya kutoa Mifupa kwenye kidali cha Kuku/How to Debone a Chicken Breast

Wakati mwingine mtu anaweza kuhitaji kupika nyama ya kuku isiyo na mifupa, mfano mzuri ni 'chicken fried rice' ambayo ilielezewa jinsi ya kuandaliwa kwenye post iliyopita. Kama ndo hivyo hata usiwaze sana kwa sababu leo utajifunza jinsi ya kufanya hivyo na ni rahisi sana.
  • Weka kidali kwenye ubao wa kukatia upande wa ngozi ukiwa juu.
  • Tumia kisu kikali kukata katikati ya kidali hadi ukutane na mfupa uunganishao upande wa kushoto na ule wa kulia. Vunja kwa nguvu upande wa juu wa mfupa na tumia kisu kutenganisha pande mbili za kidali.
  • Tumia kisu na kidole kukata nyama juu ya mfupa hadi utakapotenganisha mfupa na nyama. Fanya hivyo kwa vipande vyote viwili. Baada ya hapo unaweza kutumia nyama kupika mishkaki au chakula kingine chochote na ile mifupa kutengeneza supu. 
Ili kuelewa zaidi angalia video hapa chini.
To learn hoe to easily debone a chicken breast please watch the following video.
                   

No comments:

Post a Comment