Kawaida watu wengi huanza tu ufugaji bila kufata kanuni zozote au kuangalia kama mazingira yanayowazunguka yanaruhusu. Kwa nchi zilizoendelea kuna kanuni kabisa na sheria zinazoelekeza jinsi ya watu kufuga. Kwahiyo leo nmeandaa kanuni tano ambazo mtu anaweza kufata anapotaka kufuga kuku.
Here are five things to be aware of before you embark on your chicken keeping journey.
- Majirani/Neighbours: Kabla hujaanza ufugaji hakikisha hutosababisha usumbufu wowote kwa jirani zako. Mara nyingi watu huwa wanafuga kuku na kuwaachia tu kiasi kwamba hao kuku wanakuwa kero na usumbufu kwa majirani. Wanachafua vibaraza vya watu, wanakula chakula na nafaka, wanaharibu vitu. Mfugaji anatakiwa kuhakikisha hasababishi usumbufu kama huu kwa kuchukua hatua kama kuwajengea kuku wake uzio.
- Wanyama na wadudu/Vermin: Chakula na maji kwa ajili ya kuku vikiachwa ovyo ovyo huvutia wanyama wadogo wadogo na wadudu kama panya na mende. Hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya. Kwahiyo wafugaji hasa wanaofuga kienyeji wanatakiwa kuhakikisha chakula cha kuku hakiachwi ovyo.
- Harufu/Odour: Kinyesi cha kuku kinatoa harufu kwahiyo ni vizuri kuwa na mpango mzuri wa kufanya usafi kwenye mabanda ya kuku na kuhifadhi vizuri kinyesi cha kuku, mbali na majirani kabla ya kukitumia kama samadi ili kutokuwasumbua na harufu mbaya.
- Kelele/Noise: Kuku hasa majogoo ya kienyeji wanawika sana asubuhi na kama wanafugwa kwa wingi zile kelele zinaweza kuleta usumbufu kwa majirani. Ni wajibu wa mfugaji kuhakikisha majirani zake wako 'comfortable' kwa kutafuta njia za kupunguza kelele kufika kwao.
- Ufugaji bora/Chicken welfare: Mfugaji ahakikishe anao uwezo wa kuwahudumia kuku kikamilifu, kuwapa chakula na maji, malazi, kuwatibu wanapopata magonjwa na kuwakinga na hatari zote zinazoweza kutokea.
Hizi ni kanuni chache tu ambazo mfugaji anaweza kuzifata katika safari yake ya ufugaji, japokuwa yapo mambo mengi tu ya kuzingatia ambayo watu wengi huwa tunayapuuza. Hebu tuanze kuufikiria ufugaji kivingine ili faida iongezeke na amani pia.
No comments:
Post a Comment