Mara nyingi tumezoea kula viporo (chakula kilicholala) lakini mtu anaweza kuamua kuwa tofauti. Badala ya kuupasha tu wali uliolala anaweza kuandaa 'chicken fried rice' na kuonekana kaandaa chakula kingine kabisa tofauti na kile kilicholiwa siku iliyopita.
Mahitaji:
-Kidali cha kuku 1
-Wali uliopikwa na kukaa siku nzima (Kiporo) vikombe 5
-Mafuta ya kula vijiko 4
-Kitunguu 1
-Kitunguu saumu 1
-Karoti 1
-Pilipili hoho 1/2
-Bizari kijiko kidogo 1
-Pilipili manga kijiko kidogo 1
-Green beans
-Chumvi kijiko kidogo 1
-Njegere kikombe 1
-Mayai 2
-Soy sause kijiko kidogo 1
-Vitunguu vya kijani
Jinsi ya kuandaa:
-Pika wali kisha uache upoe au tumia kiporo.
-Andaa vipande vya nyama ya kuku visivyokuwa na mifupa.
-Changanya vipande vya kuku na pilipili manga, bizari na chumvi. Changanya hadi uwiano uwe sawa.
-Weka sufuria jikoni kisha kaanga nyama ya kuku hadi iwe ya kahawia. Ikiiva, weka pembeni na funika vizuri isipoe.
-Bandika sufuria jikoni weka kitunguu maji, kitunguu saumu,
njegere zilizochemshwa, pilipili hoho, green beans na carrot. Geuza geuza kwa muda wa dakika
2.
-Pasua mayai, mwagia kwenye sufuria kisha koroga haraka haraka ili vichanganyike na yaive vizuri.
-Ongeza wali koroga ili kuchanganya vizuri, weka kuku, endelea kukoroga takribani dakika 2 hadi 3.
-Ongeza soy sause kwenye chakula, koroga vizuri ichanganyikane na chakula
mpaka maji maji yakauke kwenye chakula na wali uwe na rangi ya kahawia.
-Pakua chakula na ukipambe uwezavyo tayari kwa kuliwa.
Chicken fried rice is a simple dish to make it may give the left over rice another delicious taste avoiding wastage by just throwing it away.
Ingredients:
-1 chicken breast
-5 cups previously cooked or left over rice
-4 tablespoons vegetable oil
-1 chopped onion
-1 teaspoon Ground garlic
-1 chopped carrot
-1/2 bell pepper
-1 teaspoon cummin powder
-1 teaspoon black pepper
-1 teaspoon salt
-1 cup boiled peas
-2 eggs
-Green beans
-Green onions
Instructions:
-Cook rice and leave it to cool or use left over rice.
-De-bone the chicken breast and cut it into small pieces.
-Mix evenly the chicken, cumin powder, black pepper and salt.
-Fry the chicken till golden brown then cover it and put aside.
-Fry onions, garlic, carrot and peas in a saucepan for 2-3 minutes.
-Add bitten eggs and keep stirring till cooked.
-Add the rice, chicken and keep mixing.
-Add soy sauce and cook till all the water is dry.
-Garnish the food and serve.