Thursday, April 7, 2016

Je Wajua: Faida za Maini ya Kuku/Did You Know: Benefits of Chicken Liver

Watu wengi tunapokula nyama ya kuku huchagua vipande vile vyenye minofu mingi kama paja, kidali na firigisi ila maini huwa hayapewi kipaumbele kabisa. Watu wengine hawapendi ladha yake. Lakini maini yana faida kubwa sana kiafya, kiufupi ni kwamba ini ni moja kati ya sehemu ya virutubisho kuliko sehemu nyingine yoyote kwenye mwili wa kuku.
 Image result for chicken liver

Virutubisho vipatikanavyo kwenye maini ya kuku:
  • Protein inayosaidia kwenye ukuaji, kuimarisha misuli, kucha, nywele na ngozi.
  • Kalsiam na phosphorus vinavyotengeneza mifupa na kuiimarisha, meno na fizi.
  • Madini ya iron yanayosaidia kuimarisha damu, kinga ya mwili na usambazaji wa oxygen mwilini.
  • Vitamini B aina zote hasa B12 ambayo ni adimu na folate ambayo husaidia kuimarisha mfumo wa uzazi wa mwanamke. Vilevile Vitamini B12 huimarisha kumbukumbu na ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu.
  • Cholesterol muhimu aina ya HDL katika utengenezaji wa testosterone, homoni ya kiume inayosaidia katika ukuaji kwa ujumla kwa wanaume.
Hata hivyo haishauriwi kula maini ya kuku kupita kiasi kwani yana cholesterol inayoweza kuwa hatari mwilini.

Although chicken breast and thighs are the most sought after pieces of chicken, chicken liver is one of the most nutritious one.

Chicken Liver Nutritional Benefits
  • Chicken liver is a good source of protein, various vitamins and minerals. Protein from the liver strengthens your muscles and offers you strong nails, shiny hair and supple skin.
  • Calcium helps strengthen your bones and teeth. Phosphorus also promotes healthy teeth, gums and bones.
  • Iron, an important mineral which improves blood constitution and supply of oxygen to bodily organs. This helps improve immunity.
  • Chicken liver is an excellent source of various B vitamins.Especially vitamin B12 and folate. Folate promotes fertility in women and helps avoid structural defects in the fetus. B12 and other B vitamins enhance the function of the nervous system, boost your energy levels and improve your physical and mental health.
  • Chicken liver, being a good source of essential cholesterol (HDL) enhances the production of testosterone in men, an important hormone which is crucial for a man's overall health.
Excessive consumption of chicken liver can prove to be harmful for some as it also provides bad cholesterol.
 
 

 

Wednesday, April 6, 2016

Vijue Vipande vya Kuku kwa Majina/Know the Chicken Parts by Names

Mara nyingi ukienda supermarket kununua kuku unakuta wanauzwa kwa vipande vipande, hivyo ni vizuri kuyafahamu majina ya vipande hivyo ili ununue kile unachokitaka. Hii inaweza kusaidia pia hata hotelini ambapo siku hizi menyu nyingi ni za kiingereza.

Here are the chicken parts and their names:
 
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_chickens.jpg
Kuku mzima: Kuku mwenye vipande vyake vyote kabla hajakatwa katwa
Whole chicken: A chicken with it’s all parts intact
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/boiler_halves.jpg
Kuku nusu: Hiki ni kipande cha kuku mzima kilichokatwa katikati.
Chicken half: A chicken is split in half lengthwise making two equal parts
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/broiler_breast_quarter.jpg
Kidali: Hiki ni kipande kinachotokana na nusu kuku iliyokatwa vipande viwili. Upande huu wenye kipapatio huitwa kidali.
Breast quarter: A chicken half cut into two pieces makes a breast quarter
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_chicken_wing.jpg
Kipapatio
Chicken wing
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_boiler_leg.jpg
Nusu ya paja: Hivi ni vipande viwili vilivyoungana
Whole chicken leg: is the drumstick-thigh combination
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/boiler_drumsticks.jpg
Paja
Drumstick
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/giblets.jpg
Shingo, ini, firigisi na moyo.
Giblets: A combination of the neck, liver, heart and gizzard.


Sunday, March 20, 2016

Mapishi: Mayai ya Kuoka/Oven Scrambled Eggs

Hii ni njia ya kuandaa mayai kwa ajili ya kifungua kinywa inayotumia zaidi na watu wa magharibi. Ni njia nzuri kwetu sisi ili kuleta ladha zaidi mpya mezani na kuipa familia afya bora.
Mahitaji:
-Siagi iliyoyeyushwa vijiko 2
-Mayai 6
-Chumvi nusu kijiko
-Maziwa nusu kikombe
Jinsi ya kuandaa
-Washa jiko la kuokea (oven) liwe na joto la 175 C au kama unatumia jiko la mkaa liandae kabisa.
-Vunja mayai weka kwenye bakuli na yachanganye vizuri pamoja na chumvi. Weka maziwa changanya vizuri.
-Weka siagi kwenye sufuria au chombo maalum cha kuokea, mimina mchanganyiko wa mayai na oka kwa dakika kumi bila kufunika.
-Geuza geuza halafu rudisha kwenye oveni oka kwa dakika nyingine kumi au hadi mayai yaive.

Preparing oven scrambled eggs is simple and the food is very nutritious even though it is not commom in Tanzania.
Ingredients:
-2 tablespoons butter
-6 eggs
-1 teaspoon salt
-1/2 a cup milk
Instructions:
-Pre-heat the oven to 175 C
-Pour melted butter into a baking dish. In a large bowl, whisk together eggs and salt until well blended. Gradually whisk in milk. Pour egg mixture into the baking dish.
- Bake uncovered for 10 minutes, then stir, and bake an additional 10 minutes, or until eggs are set. Serve immediately.


Saturday, March 19, 2016

Funny!

Hebu angalia video hii na we ufurahi kidogo.

                  

Wednesday, March 16, 2016

Jinsi ya kutoa Mifupa kwenye kidali cha Kuku/How to Debone a Chicken Breast

Wakati mwingine mtu anaweza kuhitaji kupika nyama ya kuku isiyo na mifupa, mfano mzuri ni 'chicken fried rice' ambayo ilielezewa jinsi ya kuandaliwa kwenye post iliyopita. Kama ndo hivyo hata usiwaze sana kwa sababu leo utajifunza jinsi ya kufanya hivyo na ni rahisi sana.
  • Weka kidali kwenye ubao wa kukatia upande wa ngozi ukiwa juu.
  • Tumia kisu kikali kukata katikati ya kidali hadi ukutane na mfupa uunganishao upande wa kushoto na ule wa kulia. Vunja kwa nguvu upande wa juu wa mfupa na tumia kisu kutenganisha pande mbili za kidali.
  • Tumia kisu na kidole kukata nyama juu ya mfupa hadi utakapotenganisha mfupa na nyama. Fanya hivyo kwa vipande vyote viwili. Baada ya hapo unaweza kutumia nyama kupika mishkaki au chakula kingine chochote na ile mifupa kutengeneza supu. 
Ili kuelewa zaidi angalia video hapa chini.
To learn hoe to easily debone a chicken breast please watch the following video.
                   

Monday, March 14, 2016

Uandaaji wa Banda la Vifaranga/Preparing a Brooder

  • Banda la kuku ni sehemu muhimu sana ya ufugaji wa kuku kwa sababu vifo vingi hutokea kwa vifaranga. Ni muhimu kuwa makini sana wakati wa uandaaji wa banda la vifaranga na kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanazingatiwa.
  • Banda linaweza kujengwa kwa matofali au mbao. Ukubwa wa banda unategemea idadi ya vifaranga, kifaranga mmoja anahitaji takribani 1/2 futi ya mraba.
  • Banda lipuliziwe dawa ya kuua vijidudu masaa 24 kabla ya kuwasili kwa vifaranga.
  • Pumba za mpunga au maranda ya mbao yatandazwe kwenye sakafu ya banda kisha kuwekwe magazeti juu ambayo huwasaidia vifaranga kutembea tembea kuifata sauti ya magazeti hivyo kukifikia chakula na kukila.
  • Kuwe na chanzo cha joto katika banda kama vile balbu za umeme, jiko la mkaa, mafuta au gesi kwa ajili ya kutoa mwanga na joto (takribani 95F) katika banda.
  • Nunua vifaa vya kulishia na maji kwa ajili ya vifaranga, vifaa vya maji visiwe vikubwa kuzuia vifaranga kuzama. Vifaa visafishwe vizuri kabla ya kuanza kutumika hata kama ni vipya.
 
  • As you may know, a brooder is one of the most important keys to raising chicken successfully since many deaths happen to chicks. It is very important to carefully prepare a brooder. 
  • A brooder may be made of bricks or wood. The size depends on the number of chicks wone wants to raise, one chicks requires about 1/2 a square foot.
  • A brooder should be fumigated 24 hours before the arrival of chicks.
  • Cover the brooder floor with wood chips or rice peels then put newspapers on top to encourage chicks to walk following the sound they make after stepping on the papers and find their food.
  • Provide heat by using a lamp, stove or electric bulbs.
  • Provide feeders and water-ers that are for chicks to avoid drowning (when the water-ers are too big) and they should be thoroughly cleaned even if they are new.