Monday, February 29, 2016

Fun Facts About Chicken

  1. There are more chickens than people on the Earth.    

    Kuna kuku wengi zaidi ya watu duniani. 

    Kuku wanakadiliwa kuwa bilioni 25 duniani wakati watu wanafikia bilioni 7.

      

    2. Chickens have a great memory. They can distinguish among more than 200 members of their species  

    Kuku wana uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu. 

    Inasemekana kuku mmoja anaweza kukumbuka na kuwatofautisha kuku wengine zaidi ya 200. Uwezo huu ni mkubwa kuliko ule wa tembo

     
    Fluffy chick CC0

    3. Chickens communicate and they have a full colour vision.

        Kuku wanawasiliana na wanaweza kutofautisha rangi  

    Kama ilivyo kwa binadamu, kuku wanaweza kutofautisha rangi na wana lugha ya mawasiliano. kila sauti wanayotoa ina maana. Kwahiyo wanaweza kutahadharishana kunapokuwa na hatari, kuelekezana. 

                            

    4. Chickens dream when they sleep

        Kuku huota kama binadamu wakilala

     Image result for chicken sleeping 

    5. Cocks will attempt to woo hens by performing a little dance, called “tidbitting”.

    Majogoo wana tabia ya 'kutongoza'.

    Majogoo huwatongoza majike kwa kujaribu kucheza mchezo spesho unaoitwa tidbitting kwa kiingereza. Inasemekana majike wanawapenda zaidi majogoo wenye kideli kikubwa.

     

    Image result for chicken wattle 

    6. Mother hens talk to their unborn babies.

        Kuku huongea na vifaranga kabla hawajatotolewa

    Kuku jike ana uwezo wa kuongea/kuwasiliana na kifaranga chake kikiwa bado kwenye yai kama ilivyo kwa mama na mtoto.

     

    7.  Chickens have pain receptors, enabling them to feel pain and distress.

    Kuku wanapata maumivu wanapoumia.

    Kwa sababu wana vipokeo vya maumivu katika miili yao, basi huwa wanayasikia. So unaweza kupata picha ni kiasi gani wanaumia wanapokatwa midomo bila kuchomwa sindano ya ganzi wala nini au wanapobebwa wakiwa wameshikiliwa mabawa.

      

    8. Hens defend their young from predators

        Kuku hulinda vifaranga vyao kutokana na mashambulizi

    Kuku mwenye vifaranga siku zote huwa ni mkali sana, anavilinda vifaranga vyake kutokana na mashambulizi yote yawe ya binadamu au ndege na wanyama wengine. mothersknowbest hahah

     

    9.  Chickens love to play and will run, jump and dust baths when given the chance.

    Kuku wanapenda kucheza, kurukaruka, kuoga mchanga. 

    Kuku wengi wakipata nafasi wanapenda kucheza na hata kuoga mchanga. Kuku wanaofungiwa wana-'miss' sana kujimwagia mchanga kwa sababu wanaamini wanakuwa wachafu wasipooga mchanga na mchanga unawasaidia kuua vijidudu kwenye mabawa.

      

    10. Chickens don't pee.  It is just mixed into the poop.

    Kuku hawakojoi, maji maji ya mwilini mwao yanatoka pamoja na haja kubwa.

    I hope you have enjoyed the ten fun facts about chicken and umejifunza kitu kipya especially not to hurt them kwa sababu maumivu wanayasikia.



     





2 comments: