Thursday, April 7, 2016

Je Wajua: Faida za Maini ya Kuku/Did You Know: Benefits of Chicken Liver

Watu wengi tunapokula nyama ya kuku huchagua vipande vile vyenye minofu mingi kama paja, kidali na firigisi ila maini huwa hayapewi kipaumbele kabisa. Watu wengine hawapendi ladha yake. Lakini maini yana faida kubwa sana kiafya, kiufupi ni kwamba ini ni moja kati ya sehemu ya virutubisho kuliko sehemu nyingine yoyote kwenye mwili wa kuku.
 Image result for chicken liver

Virutubisho vipatikanavyo kwenye maini ya kuku:
  • Protein inayosaidia kwenye ukuaji, kuimarisha misuli, kucha, nywele na ngozi.
  • Kalsiam na phosphorus vinavyotengeneza mifupa na kuiimarisha, meno na fizi.
  • Madini ya iron yanayosaidia kuimarisha damu, kinga ya mwili na usambazaji wa oxygen mwilini.
  • Vitamini B aina zote hasa B12 ambayo ni adimu na folate ambayo husaidia kuimarisha mfumo wa uzazi wa mwanamke. Vilevile Vitamini B12 huimarisha kumbukumbu na ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu.
  • Cholesterol muhimu aina ya HDL katika utengenezaji wa testosterone, homoni ya kiume inayosaidia katika ukuaji kwa ujumla kwa wanaume.
Hata hivyo haishauriwi kula maini ya kuku kupita kiasi kwani yana cholesterol inayoweza kuwa hatari mwilini.

Although chicken breast and thighs are the most sought after pieces of chicken, chicken liver is one of the most nutritious one.

Chicken Liver Nutritional Benefits
  • Chicken liver is a good source of protein, various vitamins and minerals. Protein from the liver strengthens your muscles and offers you strong nails, shiny hair and supple skin.
  • Calcium helps strengthen your bones and teeth. Phosphorus also promotes healthy teeth, gums and bones.
  • Iron, an important mineral which improves blood constitution and supply of oxygen to bodily organs. This helps improve immunity.
  • Chicken liver is an excellent source of various B vitamins.Especially vitamin B12 and folate. Folate promotes fertility in women and helps avoid structural defects in the fetus. B12 and other B vitamins enhance the function of the nervous system, boost your energy levels and improve your physical and mental health.
  • Chicken liver, being a good source of essential cholesterol (HDL) enhances the production of testosterone in men, an important hormone which is crucial for a man's overall health.
Excessive consumption of chicken liver can prove to be harmful for some as it also provides bad cholesterol.
 
 

 

Wednesday, April 6, 2016

Vijue Vipande vya Kuku kwa Majina/Know the Chicken Parts by Names

Mara nyingi ukienda supermarket kununua kuku unakuta wanauzwa kwa vipande vipande, hivyo ni vizuri kuyafahamu majina ya vipande hivyo ili ununue kile unachokitaka. Hii inaweza kusaidia pia hata hotelini ambapo siku hizi menyu nyingi ni za kiingereza.

Here are the chicken parts and their names:
 
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_chickens.jpg
Kuku mzima: Kuku mwenye vipande vyake vyote kabla hajakatwa katwa
Whole chicken: A chicken with it’s all parts intact
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/boiler_halves.jpg
Kuku nusu: Hiki ni kipande cha kuku mzima kilichokatwa katikati.
Chicken half: A chicken is split in half lengthwise making two equal parts
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/broiler_breast_quarter.jpg
Kidali: Hiki ni kipande kinachotokana na nusu kuku iliyokatwa vipande viwili. Upande huu wenye kipapatio huitwa kidali.
Breast quarter: A chicken half cut into two pieces makes a breast quarter
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_chicken_wing.jpg
Kipapatio
Chicken wing
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/whole_boiler_leg.jpg
Nusu ya paja: Hivi ni vipande viwili vilivyoungana
Whole chicken leg: is the drumstick-thigh combination
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/boiler_drumsticks.jpg
Paja
Drumstick
http://www.chicken.org.au/files/_system/Image/FoodInformation/Cuts/giblets.jpg
Shingo, ini, firigisi na moyo.
Giblets: A combination of the neck, liver, heart and gizzard.